Jumamosi, 6 Juni 2015

MWALIMU MWANAFUNZI (USHAIRI)

NA RICHARD, KASHINJE 0764711129
rkashinje@gmail.com

MWALIMU MWANAFUNZI

1          Mwalimu uwe makini, makini kumakinika
Mwalimu si masikini, akilize kulabuka.
Walimu sikilizeni, yamoyo yalotukuka
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo.

2          Siku uwapo kazini, kusoma huna kikomo
Hata kama nimezani, kitabu hakina komo
Pata yawanazuoni, mapya kwako yaliyomo
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

3          Usishike mazoea, kusoma moja pekee
Kusema umebobea, hakika si wapekee
Kazi yako watachukua, waliosoma pekee
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

4          Usipokuwa msomi, tena wakusoma sana
Wanafunzi hawakusomi, kwako ni aibu sana
Hawatakupenda msomi, na hiyo fedheha sana
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

5          Kumbuka ile kauli, ambayo kwetu nirai
Mwalimu kuwa mkali, wanafunzi kuzirai
Kwako murua kauli, kwao somo wafurai
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

6          Siku zimebadilika, yakupasa utambue
Wanafunzi huzunguka, ukweli wautambue
Yakupasa kumakinika, wasomi wasiumbue
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo.

7          Msomi tulikuamini, tuakukabidhi kazi
Kwakuwa niutamaduni, nzuri ufanyapo kazi
Pia tuanatatumaini, kazi iota mizizi
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

8          Kusoma hana kikomo, mwalimu ni mwanafunzi
Mwanafunzi hana komo, kusoma ni mwanafunzi
            Haya ndani yawe yamo, kazi ni uwanafunzi
Mwalimu ni mwanafunzi, kusoma hana kikomo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni