Jumamosi, 6 Juni 2015

MIIKO YA KABILA LA WAKEREWE

Falsafa nidhana nyeti sana katika maissha  na utamaduni wa wabantu waishio katika bara la Afrika. Katika kujadili swali hili tutaanza kujadili dhana za Falsafa jinsi ilivyoelezwa na wataalamu mbalimbali, tutaleleza maana ya miiko jinsi ilivyoelezwa na vyanzo mbalimbali, tutaeleza historia fupi ya wilaya ya Ukerewe, tutaeleza kiini cha swali letu ambapo tutakeleza miiko mbalimbali ambayo inapatikana katika kabila la Wakerewe na hatimaye tutahitimisha kwa kutoa tathimini ya miiko hiyo kwa sasa jinsi inavyochukuliwa. Tuanze kwa kuziangalia maana mbalimbali za Falsafa jinsi ilivyojadiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;
http://sw.wikipedia.org/wiki/Falsafa Falsafa ni jaribio la kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayofuata njia ya mantiki kwa kuchunguza mambo kama kuweko na kutokuweko, ukweli, ujuzi, uzuri, mema na mabaya, lugha, haki na mengine yoyote.
http://pengotz.blogspot.com/2007/12/falsafa-ya-elimu-tanzania.html wanaeleza kuwa, falsafa ni taaluma inayojishughulisha na kutafuta ukweli wa jambo kwa njia ya kutafakar.
Kwa ujumla tunaweza kuseama kuwa, Falsafa ni tawi la sanaa ambalo linajishughulisha na kutafuta ukweli wa mambo jinsi yalivyo kwa njia ya fikra na tafakuri za hali ya juu juu ya mambo hayo ambayo ni ukweli, mantiki, kuwepo na kutokuwepo kwa mambo.
Baada ya kueleza maana ya Falsafa jinsi ilivyoelezwa hapo juu sasa tuziangalie maana za  miiko jinsi zilivyojadiliwa navyanzo mbalimbali kama ifuatavyo;
en.wikipedia.org/wiki/Taboo Miiko ni makatazo makali ya matendo yaliyo katika imani ya tabia ambayo pengine ni takatifu sana au laana sana kwa mtu binafsi wa kawaida kufanya chini ya tishio ya adhabu isyo ya kawaida. (tafsiri yetu)
www.wisegeek.com/what-is-a-taboo.htm  Mwiko ni kukataza dhidi ya shughuli fulani, kwa kawaida mizizi katika imani za kitamaduni au maadili. Vitu, watu, na maeneo pia inaweza kama mwiko ilivyoelezwa, kwa maana ya kuwa wao ni haramu au kwamba sheria maalum zinazowazunguka wao.
www.oxforddictionaries.com/definition/english/taboo Miiko kijamii au kidini na desturi ni kukataza au kuzuia vitendo fulani au akipinga kushirikiana na mtu fulani, mahali, au jambo.
Hivyo, miiko ni makatazo ambayo jamii huyaweka na kuyatilia adhabu kali kwa mtu yeyote ambaye angeweza kukaidi maagizo hayo.
Baada ya kumaliza kueleza maana ya miiko sasa tuiangalie historia ya wilaya  ya Ukerewe  ambamo ndimo miiko yetu tuliyoijadili ndimo ilimotoka kama ifuatavyo;
https://envaya.org/lakevictoriachildren_lvc/history wanaeleza  kuwa, Ukerewe ni kisiwa kubwa katika Ziwa Victoria ambacho ni kubwa ya kitropiki na ni cha  pili kwa ukubwa  katika maziwa yenye maji baridi  duniani. Kisiwa hiki kina ukubwa wa eneo la 6400 km2.  nchi kavu ina  640 km2 ni nchi na wengine 5760 km2 ni maji ya Ziwa Victoria Kuna visiwa 38 kisiwani Ukerewe kambapo makao makuu yake ni wilaya ya  Nansio . Kati ya visiwa 38, visiwa 15 ni ya kudumu na hutumika kwa makazi wakati vinavyobaki hutumika kama makazi yamda kwa wavuvi . Wilaya iko kusini mwa Wilaya Ilemela na Magu. Mashariki kuna Wilaya  Bunda na Musoma katika Mkoa wa Mara, kwa kusini magharibi inapakana na Wilaya ya Sengerema, kwa magharibi mkoa wa Kagera na kaskazini Jamhuri ya Kenya na Uganda
baada ya kumaliza kueleza historia ya wilaya ya ukerewe ifuatayo ni miiko inayopatikana katika wilaya ya ukerewe katika kabila la wakerewe.
1)      Nimarufuku kwa mtoto wa kiume kukaa jikoni, maana yake ni kuwa, nguo za mama yake zinaweza kuvuka akaona uchi wa mama yake. Lakini maana yake halisi ni kuwa kama mtoto wa kiume angekaa jikoni angeliweza kuunguo
2)      Nimarufuku kuua chatu. Maana yake kwani ni unauugua bila kupona na hadi kufa. Lakini ni kwamba chatu alikuwa amefugwa na mtemi wa wakerewe.
3)      Nimarufuku mwanamke kutaja baba mkwe wake kwa jina lake au jina linalofanana na la baba mkwe wake. Maana yake ni kutunza heshima na badala yake mwanamke alitafta tafsida ya jina hilo ndiopo amuite baba mkwe wake.
4)      Nimarufuku kwa mtu yeyote kuanza kuchimba kaburi la mtualiyefariki  mwenye magonjwa  kama kifafa, kichaa mpaka ndugu yake aanza kuchimba ndipo wengine wafuatie. Hii ikikiukwa watu hao watauugua  mpaka kufa. Na suluhu yake ni kwamba mazindiko hufanywa ili kuhakikisha marehemu anazikwa na magonjwa yake.
5)      Nimarufuku kwa bibi harusi kukatisha katikati ya uwanja wa kaya. Hii ni kwa sababu katikati ya uwanja ndipo baba nyenywe nyumba alipokuwa akiotea moto kwa hiyo angeliweza kumuona akiwa uchi.
6)      Nimwiko kwa mwanamke aliyeolewa kula na baba mkwe wake meza moja.  Hii ilikuwa ni kwa sababu wanaume wanakula haraka na wanawake wanakula taratibu hivyo waliogopa mkwe wao kutokushiba.
7)      Nimwiko kwa mwanamke kula nyama ya kuku au mayai yake kwa kuogopa kuwa watoto wangekuwa na tabia za kula kila kaya. Lakini maana yake ya ndani ni kuwa; kwakuwa wakerewe ni wafugaji  wa kuku kwahiyo waliogopa kuku wao kumalizwa na mama wakati wa ujauzito.
8)      Nimarufuku kwa  mtoto yeyote kukalia kinu kama akikalia kinu hatakua lakini maana yake ni kwamba ikiwa mtoto akikalia kinu angeweza kutoa ushuzi na hatimaye kuchafua kinu ambacho ni chombo cha kutwangia nafaka.
9)      Nimarufuku kwa mwanaume kula na mama mkwe wako. Kwani angweza kumlaza njaa lakini maana yake ni kwa nguo za mama mkwe wake zingeweza kuanguka na kumuona uchi wake.
10)  Nimarufuku kwa wanaume katika familia kula meza moja na wanawake kwani nguo zingaliweza kuanguka na kuwaona dada zake na mama zake uchi. Lakini ni kwamba mwanamke anakula taratibu na mwanaume anakula haraka haraka hivyo waliogopa kuwalaza njaa wanawake.
11)  Nimarufuku kwa mkerewe kula ndege aina ya nfunzi kwani ataugua ugonjwa wa kuvuka ngozi ya juu na ngozi ya ndani kuja juu. Lakini maana yake ni kuwa kwa kuwa ndege huyo alikuwa natumika katika kufanyia shughuli za kiganga hivyo waliogopa kuruhusu ndege hao wasilike ili wasije wakaisha mana hata upatikanaji wake ni adimu sana.
Kwa kuhitimisha tunaweza kutoa tathimini ya miiko hiyo na jinsi ilivyo kwa sasa. Mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka ya tisini miiko ilikuwa bado ina mashiko na ilikuwa ikifanya kazi na watu waliieheshimu. Lakini baada ya kuingia kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliyosukumwa na utandawazi miiko mingi ya wabantu imekufa kwa kuwa mambo siku hizi yanapelekwa kizungu na kwa hali hii kuna hatari ya miiko kufa na kupotea kabisa . hivyo juhudi za ziada zinahitajika sana ili kuweza kuzilithisha katika vizazi vijavyo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuandika miiko ili kuzitunza kwa mstakabali wa maisha ya baadaye.


MAREJELEO
http://pengotz.blogspot.com/2007/12/falsafa-ya-elimu-tanzania.html imepakuliwa tarehe 13/04/2015 saa 4:48 asubuhi
en.wikipedia.org/wiki/Tabo  imepakuliwa tarehe 14/04/2015 saa 2:16 usiku

http://sw.wikipedia.org/wiki/Falsafa. Imepakuliwa tarehe 13/04/2015 saa 4:18 asubuhi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni