Naratolojia
ni dhana inayolejelea usimuliaji katika kazi za kifasihi; huweza kupambanua
matukio mbalimbali kwa uwazi au la kutokana na aina ya usimuliaji. Huweza
kujenga uelewa wa maudhui kama usimuliaji ulikuwa wa moja kwa moja na wa wazi
au huweza kufanya maudhui kutoeleweka kwa wazi kama usimuliaji huakuwa wa wazi.
Mfano katika kitabu cha Mzingile kilichoandikwa
na E. Kezilahabi. Vile vile kipengele hiki cha usimulizi ni muhimu kwani ndicho
ambacho hubainisha mwendo katika kazi husika, pia huweza kuonyesha nafasi ya
uwakati katika kazi husika.
Kuna
aina kuu mbili za usimulizi katika kazi za kifasihi (hasa fasihi andishi) ambao
ni usimulizi shahidi ambazo katika usimuliaji wake hutawaliwa na matumizi ya
nafsi ya kwanza kwa kiasi kikubwa. Pia huweza kuhusisha matumizi ya nafsi ya
pili. Huu ni usimulizi bora kwani husimulia mambo ambayo msimuliaji ana uhakika
nayo kwani mara nyingi huwa yamemtokea au kuyaona yeye mwenyewe. Kwa kuwa
husimulia mambo mengi, pia huweza kuufanya mwendo wa kazi husika kwa wa
polepole.
Pia
kuna usimulizi maizi ambao hutumia nafsi ya tatu katika kusimulia. Huweza
kuruka baadhi ya mambo na hata kufanya mwendo wa kazi husika kuwa wa kasi kwa
sababu msimuliaji husimulia mambo ambayo kwa namna moja au nyingine husimulia
mambo ambayo hayajampata yeye au kuyashuhudia kwa macho yake na badala yake
huwa amesimuliwa tu.
Katika
kitabu hiki cha Msako aina hizi zote
za nafsi zimetumika kwa namna tofauti tofauti. Mwandishi Naguib Mahfouz
ametumia usimulizi shahidi hasa katika dialojia nyingi kama vile katika ukurasa
wa 47 kuna matumizi ya nafsi ya kwanza umoja pale anaposema;
“Kila
nitakapojisikia kufanya hivyo…”
Pia kuna matumizi ya nafsi ya kwanza uwingi
katika ukurasa wa 51;
“Tuna
habari ya kushangaza kwa ajili yako…”
Mwandishi
ametumia nafsi ya kwanza ili kujikaribisha na uhalisi kwa kumpa mhusika maneno
na matendo ambavyo hadhira kuamini kuwa jambo linalosemwalipo kama lilivyo.
Pia
kuna matumizi ya nafsi ya pili katika kitabu cha Msako kama ilivyoonekana katika ukurasa wa 46 pale anaposema;
“Umewezaje
kuja chumbani kwangu…”
Pia
katika ukurasa wa 52 mwandishi anasema;
“Wewe ndiye mgeni, …”
Vilevile
kitabu hiki kwa kiasi kikubwa kimesheheni matumizi ya nafsi tatu umoja na uwingi kama ilivyooneshwa na
mwandishi. Mwandishi katika kukisimulia kisa chake kwa kiasi kikubwa ametumia
nafsi ya tatu umoja kama ilivyonukuliwa katika baadhi ya kurasa kama vile
katika ukurasa wa 1 pale anaposema;
“Aliudhiwa na mguso huo na kimyakimya
akamlaani huyo aliyemgusa. Mtu huyo ni nguruwe kama …”
Pia
katika ukurasa wa 50 mwandishi anadhihirisha hilo pale naposema;
“Alizinduka huku kijasho chembamba kikimtoka, akipumua kwa nguvu.
alikuwa kwenye chumba chake pale hotelini…”
Pia
kuna matumizi ya nafsi ya tatu uwingi kama vile katika ukurasa wa 112 pale
anaposema;
“Walimkuta
na fedha zilizoibwa.”
Hivyo
katika kazi hii matumizi ya nafsi zote yametumika katika kuisimulia kazi hii.
Hata hivyo kwa kiasi kikubwa mwandishi Naguib Mahfouz ameonekana kuegemea zaidi
katika matumizi ya nafsi ya tatu umoja kwa sababu kadhaa lakini kubwa zaidi ni
kutaka………
MWENDO
Mwendo
ni mtiririko hasi na mshindilio wa vitushi katika riwaya kwa kuzingatia msuko,
masafa ya wakati na masafa ya kijiografia. Mwendo wa riwayahusika hujengwa na
msuko wa vitushi, maudhui, masafa ya kiwakati na ya kijiografia. Hivyo kupitia
vipengere hivi msomaji wa riwaya husika
ataweza kung’amua mwendo wa kazi husika. Kutokana na vipengere hivi kuna aina
tatu zamwendo kama ifuatavyo;
Mwendo
wa kasi, katika mwendo huu masafa ya kiwakati huenda harakaharaka kwa maana kwamba katika shughuli nzima ya
usimulizi wa hadithi husika, muda au wakati wa matukio na matendo mbalimbali
katika kazi husika huwa ni wa
harakaharaka zaidi. Pia maudhui ya kazi zenye aina hii ya mwendo huwa ni ya
kifutuhi asilimia kubwa. mbali na maudhui, masafa ya kijiografia katika kazi
zenye aina hii ya mwendo ambayo huhusisha utajaji wa majina ya maeneo na sehemu
mbalimbali kulingana na madhari iliyotumika katika andikohusika, huwa ni wa
kimasafa ya kasi zaidi kutokana na kutajwa kwa maeneo tofauti tofauti yaliyo
mbali kijiografia. Vilevile katika mwendo huu, huwa kuna msuko wa vitushi uendao
haraka. Kwa kifupi katika aina hii ya mwendo shughulinzima ya usimulizi
hufanyika kwa kasi zaidi.
Mwendo
wa kati, mwendo huu huchanganya maudhui ya kitanzia na ya kifutuhi na katika
hali nzima ya masimulizi huchukua muda kutoka katika maudhui fulani kwenda
katika maudhui mengine. Mbali na hilo, masafa ya wakati na kijiografia husafiri
kwa wastani/taratibu kwa maana ya kwamba sio wa kasi wala wa polepole.
Pia
kuna mwendo wa polepole, sifa za mwendo huu ni kwamba, maudhui ya kitanzia
hutawala kwa kiasi kikubwa katika kazi husika, masafa ya wakati na ya
kijiografia huenda polepole, vilevile katika mwendo huu kuna sifa ya
kujilejelea kwa masimulizi na mwisho kabisa, kazi zenye aina hii ya mwendo
huwachosha wasomaji.
Kwa
jumla, riwaya ya Msako ni andiko lenye
mwendo wa wastani/kati, hii nikutokana na kukidhi vigezo na sifa za aina hii ya
mwendo kama ifuatavyo;
Suala
la maudhui, riwaya ya msako ina maudhui changamani. Hii ina maana kwamba kuna
maudhui ya kitanzia na ya kifutuhi. Kwa mantiki hii basi riwaya hii ni ya
mwendo wa kati, baadhi ya maudhui ya kitanzia yanayojitokeza katika andiko hili
ni haya yafuatayo;
Suala
la mauaji (vifo). Vifo au mauaji ni suala ambalo limezungumziwa katika riwaya
hii ya Msako kwa mfano, mwanzoni
kabisa mwa kitabu kunazungumziwa shughuli ya mazishi ya kifo cha mama yake
Suber (Basima Omran). Hali kama hii kwa hakika inaleta huzuni kwa msomaji,
ukizingatia ni suala ambalo huleta huzuni kwa wanajamii katika jamii zetu.
Katika uk.1 aya ya kwanza mwandishi anasema hivi;
“Macho yake yalijawa na machozi.
Licha ya jitihada zake dhidi ya mihemko yake na aibu aliyoihisi kulia mbele ya watu hawa kwa
kweli alizidiwa. Kwamacho yenye machozi alitazama kuelekea kwenye maiti
iliyokuwa ikiondolewa kwenye jeneza na kupelekwa kwenye kaburi lililokuwa
wazi…….”
Lakini
pia katika uk.86 suala la mauaji limejitokeza pale ambapo mhusika Suber
anachukua uamzi wa kumuua mzee Khahili kwa lengo la kumiliki mali na mwanamke
wa mzee huyu. Hivyo suala hili linaleta huzuni kwa wasomaji na hata katika
jamii kwa jumla. Katika ukurasa huo aya ya kwanza mwandishi anasema hivi;
“Aliunyanyua ule
mtarimbo. Ghafla Yule mzee alijigeuza kivivuvivu.Suber alijihisi kuganda pale
alipokuwa amesimama, mikono ikiwa imeinuliwa juu, mtalimbo juu ya kichwa chake.
Macho yao yalikutana.Suber alitambua hatari ya jambo hilo na kuachia mikono
yake ishike na kutoa pigo kali. Yule mzee alipiga ukulele mdogo, halafu
manung’uniko kidogo, kasha kimya.”
Vilevile,
dhamira nyingine yenye kuleta hali yakitanzia ni suala la kufungwa kwa watu magerezani/jela
(vifungo ). Kwa hakika ni suala ambalo linaleta huzuni kwa wasomaji
halikadhalika jamii kwa jumla pale hukumu za kufungwa jela zitolewapo watu
huuzunika japo kwa upande mwingine watuhufurahia hali hii kulingana hasa na
matukio yanayosababisha hukumu kama hizi. Kwa mfano katika uk.17 aya ya pili
mwandishi anasema;
“Yote ni kama ndoto ya
ajabu. Niliondoka Alexandria kuja huku kumtafuta baba yangu, halafu vitu vya
ajabu vilitokea ambavyo vilinisababisha kusahau lengo langu la awali na
hatimaye kunisukumia jela.”
Lakini
pia suala la kufungwa jela lilimtokea mama yake Suber (Basima Omran) pindi
alipofanya mauaji na kufungwa muda wa miaka mitano. Suala ambalo linasababisha
kifo chake punde tu alipolejea nyumbani. Hili linajidhihirisha katika uk.3 mwishoni
kabisa mwa aya ya mwisho.
Halikadhalika
kuna suala la utengano dhidi ya wanandoa, jambo ambalo lanasababisha watoto
kukua katika malezi ya upande mmoja wa uzazi. Suala hili linaonekana
kusababisha malezi na makuzi ya watoto yasio mazuri (maadili mabaya) mfano
alivyolelewa Suber, hakulelewa katika maadili mazuri kwa kulelewa na kukukzwa
katika maisha ya anasa na starehe na mwisho wake katika harakati za kumsaka
baba yake anaishia katika mikono ya nguvu za dora na kutumikia kifungo cha
maisha jela.
Lakini
pia mhusika Elhamu kakua katika malezi ya mama tu baada ya kutengana kwa mama
na baba yake kipindi bado yuko mchanga. Katika uk.54 kuanzia aya ya tatu
mwandishi anasema;
“Ninaishi na mama yangu. Familia
yetu ipo Qalyoub. Mjomba wangu anaishi Heliopolis. Na tuna mtu tuliyempoteza
katika familia yetu”. Kusema kweli wazazi wangu walitengana nilipokuwa ningali
motto mchanga….”
Mbali
na maudhui ya kitanzia kuna suala la mapenzi, ulevi, watu kujishughulisha na
shughuli mbalimbali, umuhimu wa elimu nakadhalika, dhamira ambazo zinasababisha
riwaya hii kuwa na maudhui changamani na hatimaye kukidhi vigezo vya kuwa na
mwendo wa wastani kama ilivyotambulishwa awali. Lakini pia hata suala la masafa
ya wakati na ya kijiografia, ni ya wastani kutokana na kutajwa kwa maeneo na
nyakati (madhari) mbalimbali katika hali isiyokuwa ya kasi. Kwa mantiki hiyo
basi, riwaya ya Msako ni riwaya yenye mwendo wa kati/wastani.
MTINDO
Senkoro (2001), anabainisha vipengere
vikuu vitatu vya mtindo ambavyo ni;
Mbinu za kibunilizi au utunzi, hizi ni
mbinu mbalimbali wazitumiazo watunzi katika kazi zao. Mbinu hizi ni kama vile
uingizaji wa fani mbalimbali katika utanzu unaoshughulikiwa kama vile
masimulizi, usemezano baina ya wahusika , utomeleaji motifu za safari na
kadhalika. Mwandishi wa riwaya ya Msako
kwa kiasi kikubwa amefaulu katika uteuzi wa mbinu mbalimbali za kibunilizi
mfano dayalojia, masimulizi, motifu za safari nakadhalika. Mfano wambinu
aliyoiyumia ni motifu ya safari.
Motifu
ya safari ni mbinu ya kiuandishi anayoamua kuitumia mtunzi au mwandishi kwa
lengo la kusukuma kazi mbele na kupitia msukumo huu ndipo matukio mbalimbali,
dhamira na jumbe mbalimbali, madhari na vipengere vingine huweza kujitokeza.
Kwa mfano katika uk.17 aya ya pili, mbinu hii inajidhihirisha pale Suber anapoianza
safari yake kutoka Alexandria kuelekea Cairo. Mwandishi anasema;
“Alexandria ilififia kwa mbali
kadri garimoshi lilivyoongeza mwendo kuelekea Kusini upande wa Cairo. Robo
karne yenye kumbukumbu tele ilififia mbali katika alfajiri ile ya majira ya
kipupwe, ilifunikizwa na mawingu meusi yanayotangaza…..”
Motifu
ya ndoto, hii ni mbinu ambayo mwandishi huitumia ili kusukuma mbele kazi yake.
Katika mbinu hii, licha ya kuwa mwandishi anakuwa na lengo la kupeleka mbele
simulizi lake lakini mwandishi hukusudia kufikisha ujumbe fulani kwa hadhira.
Katika riwaya ya Msako, mwandishi
ametumia mbinu hii kuanzia ukurasa wa 48-50. Katika mbinu hii tunapata dhamira
kama dharau na nafasi mwanamke katika jamii yaani, mtu mwenye kudhauliwa.
Mwandishi anasema;
‘‘Niondolee! Nisikuone tena! Wewe ni takataka tu, kama
Mama yako. Huna
chochote unachostahili toka kwangu!’’(uk. 50)
Katika
mfano hapo juu, unaonesha pale Saber alipokuwa yuko ndotoni akiwa anaota kuwa
amekutana na baba yake na akachana vyeti alivyokuwa amemuonesha kama
uthibitisho na hatinaye kumfukuza na kumtukana.
Kipengere kingine ni uteuzi wa maneno,
hiki ni kipengere muhimu sana katika mtindo wa kazi husika. Katika kukamilisha
mtindo ulio bora zaidi, mtunzi wa kazi ya anapaswa kuwa na weredi wa hali ya
juu katika kuteuwa maneno yenye uzito ili kuleta mvuto kwa wasomaji wa kazi
yake. Ufundi wa uteuzi wa maneno ndio unaofanya kazi ya mwandishi ionekane ya
pekee. Mawazo yote aliyonayo mwandishi akilini tayari yalikwisha fanyiwa kazi
na waandishi wengine, hivyo uteuzi wa manemno mazito yenye kujenga taswira,
jazanda na ishara akilini mwa msomaji ndiyo
yanayoleta upya wa kazi
yake. Mwandishi wa riwaya hii amedhihirisha hili kwa kuteuwa maneno mbalimbali.
Miongoni mwa maneno hayo ni kamavile;
“Nilichezwa machale” uk,10
“Alipiga pafu moja ndefu”
uk.7
“Alikuwa bonge la
mwanamke” uk.18
“Hakuna ninachoweza
kufanya zaidi ya kuwa gangwe, mhuni, kuwadi” uk.5
“Alistafiani kwa mayai,
jibini, bilauri ya maziwa na matunda” uk.79 n.k.
Vilevile kipengere
kingine ni matumizi ya lugha ya picha na ishara. Lugha ya picha na ishara ni
tokeo la uweredi wa mtunzi katika suala zima la uteuzi wa maneno. Uteuzi wa
maneno ndio zao la ujenzi wa taswira, picha na ishara akilini mwa msomaji.
Maneno mazuri aliyoyatumia yanaweza kumuathiri msomaji kwa kiasi ambacho
msomaji huyo anaweza kujenga taswira akilini mwake. Taswira hizo ndizo
zinazomsaidia msomaji kubaini ishara mbalimbali zinazoweza kugundua dhana ya
kitu au mtu fulani. Kwa mfano katika riwaya hii uk.18 mwandishi anasema;
“Alikuwa
bonge la mwanamke! Ghafla alijihisi kuamkwa na tamaa iliyokuwa kama imelala na
kumbukumbu za mbali zilizopotelea kwenye ukungu wa wakati.”
Maneno kama “bonge la mwanamke na kuamkwa na tamaa” ambayo yameteuliwa na
mwandishi yanamsaidia msomaji kujenga taswira ya hisi juu ya haiba ya mwanamke
aliyekutana na Suber na neno kuamkwa na
tamaa linamsaidia msomaji kuvuta picha na hali aliyokuwa nayo Suber baada
ya kukutana na mwanamke yule. Hivyo taswira kama hizo ndizo zinazoweza kuupa
msomaji picha nzima ya tukio ambalo lingeweza kutendeka kati ya Suber na
mwanamke huyo.
Matumizi
ya lugha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi, na bila yenyewe kuwepo haiwezekani
kuwepo kazi yoyote ya fasihi.Mwandishi ametumia lugha katika kuyaibua mawazo
yake katika kazi yake.Matumizi ya lugha hujumuisha
methali,misemo,nahau,taswira,lugha ya picha na ishara pamoja na tamathali za
semi.Lugha imesanwa vyema na kumsaidia mwandishi kuwa na ubunifu wa hali ya juu.Katika
riwaya hii ya MSAKO mwandishi ametumia lugha kama ifuatavyo;
Mwandishi
ametumia lugha inayoeleweka kwa urahisi na moja kwa moja.Hii haina maana kazi
imepyaya katika fani na matumizi ya lugha kwa jumla.Bali ni kuonesha ufundi
wake katika kusana lugha kifasihi kwa namna inayoeleweka kwa hadhira.Mfano
ukurasa wa 134 mwandishi ameonyesha jinsi Saber alivyokuwa jela kwa kutumia
lugha inayoeleweka kwa urahisi.
Sasa Saber uko wapi?Jela,peke yako.Hakuna
anaekutembelea.Hakuna
yeyote wa kukutembelea.
Pia
mwandishi ametumia tamathali za semi katika kazi yake.Tamathali za semi ni
viwakilishi au vifananisho vya dhana fulani kwa dhana nyingine zinazofanana au
zinazotofautiana.Ni usemi wenye kupanua, kupuuza au kubadilisha maana za
dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana nyingine.Tamathali za semi
hutia nguvu kazi ya fasihi na kuipamba.Katika riwaya hii mwandishi ametumia
sitisri,tashbiha,tashihisi,lakabu pamoja na takriri.
Kwanza,
ametumia sitiari.Sitiari ni tamathali inayounganisha vitu au watu lakini bila
ya kutumia viunganishi linganishi kama vile mithili ya, mfano wa, sawa na, na kama.Tamathali
hii huunganisha vitu na watu kana kwamba vitu na watu hao ni sawa kabisa. Mwandishi
ametumia ulinganisho wa Bwana Khalil na ibilisi mzee na mjinga pale Karima na
Saber walipokuwa wanapanga mipango ya kumuua na kutoroka. Msanii anasema
ukurasa wa 60
Yeye ni ibilisi mzee na mjinja. Mara tu
akihisi
nitaacha
kuonana na wewe.
Pia
ametumia sitiari ukurasa wa 84 kuonyesha ulinganisho wa fundi bomba na ibilisi
laghai pale Bwana Khalil alipokuwa anampa maagizo Sawi bawabu na kumsisitiza
asisahau.Msanii anasema
Yule ni ibilisi laghai. Alikaribia kufa mara
nne,
na
bado hajajifunza.
Pia
mwandishi ametumia tashbiha.Tashbiha ni tamathali inayolinganisha watu, vitu
viwili au zaidi hulinganishwa na watu ama vitu vingine kwa kutumia maneno kama
mithili, kana kwamba, mfano wa, na kama. Mwandishi ametumia tashbiha kuonyesha
Bwana Reheimy alivyomfananisha Saber na mama yake kuwa ni takataka na hana
chochote anachostahili kumiliki.Tashbiha hii imeonyesha mwanamke amechorwa kama
kiumbe duni kwa kulinganishwa na takataka. Mfano ukurasa wa 50 mwandishi
anasema
Niondokee! Nisikuone tena! Wewe ni takataka
tu,
kama
mama yako. Huna chochote unachostahiki
toka
kwangu.
Mwandishi
kwa kiasi kikubwa ametumia tashbiha katika ukurasa wa (50), (51), (53), (56), (58),
(62), (64), (73), (77), (79), (81), na (84).
Tatu,
mwandishi ametumia lakabu. Lakabu ni majina anayopewa au kujipa mtu kutokana na
sifa alizo nazo. Sifa hizo huweza kuwa za kiumbo au za kitabia. Mwandishi
ametumia lakabu ya bata mzinga wa porini kumsawiri baba yake Saber ambaye
hatulii sehemu moja.Ukurasa wa 145 mwandishi anasema kwa kumtumia mwanasheria
Wajibu wangu uko katika kuielewa kesi yako
kwa
kina na, si kumfukuza bata mzinga wa
porini.
Nne,
mwandishi ametumia takriri.Takriri ni urudiaji rudiaji wa maneno au sentensi
kwa malengo maalum ya kusisitiza. Mwandishi ametumia takriri ili kuwekea mkazo
dhamira na kuisisitiza. Takriri imejitokeza pale Sawi bawabu anapokwenda
kumuamsha Bwana Khalil chumbani kwake. Baada ya kutoitika hivyo, Sawi
akarudiarudia kugonga mlango na kuita ili kumuasha Bwana Khalil ambaye alikuwa
ameuwawa na Saber.Ukurasa wa 92 mwandishi anasema
“Bwana Khalil!Amka!Amka!Bwana Khalil
imekaribia
Saa
mbili kamili”.
Tano,
mwandishi ametumia tashihisi.Tashihisi ni tamathali ambayo vitu visivyo na sifa
walizonazo watu hupewa sifa hizo za watu.
Mwandishi ametumia tashihisi pale ambapo Saber alimgusa Elham mkono na kuhisi kila msuli ndani yake ukiimba. Kuimba
hufanywa na watu na sio msuli hivyo sifa ya kuimba ilipewa msuli. Mfano ukurasa
wa 66 mwandishi anasema
Alimgusa mkono wake na kuupigapiga taratibu.
Kila
msuli
ndani yake ulikuwa ukiimba;halafu alimkumbuka
Karima
na mpango wao wa kukutana saa chache zijazo.
Sita,
tashihisi imejitokeza ukurasa wa 3 ambapo Saber alikuwa njiani kuelekea
nyumbani ambapo alipepewa na upepo unaomburudisha na kubeba harufu nzuri. Upepo
umepewa sifa za mwanadamu;
Akiwa njiani kuelekea nyumbani upepo mwanana
unaoburudisha
ulimpepea,ukibeba pamoja nao harufu
nzuri
ya majira ya machipuko.
Vilevile,
mwandishi ametumia taswira katika kazi yake.Taswira ni picha mbalimbali
zinazojengeka akilini mwa msomaji kutokana na uteuzi na upangaji wa maneno wa
mwandishi. Lugha ya picha na ishara huchangia kwa kiasi kikubwa ujengaji wa
taswira. Mwandishi ametumia taswira pale ambapo Saber alimtazama ombaomba
vizuri na kuhisi kinyaa. Msanii anasema ukurasa wa 87;
Yule ombaomba alimpita. Kwa mara ya kwanza
aliweza
kumtazama
vizuri. Du, anatia kinyaa! Uso mwembamba,
uliokondeana,
pua kubwa na macho mekundu, kama
yaliyovilia
damu.
Pia mwandishi
ameonyesha tawsira ya harufu ya uvundo aliyokuwa anatoa yule ombaomba. Saber alipitiwa
na harufu ya ombaomba yule. Ukurasa wa 87 mwandishi anasema;
Yule ombaomba alimpita na harufu
iliyotarajiwa ya
uvundo
ambao uliendana na mwonekano wake.
Vilevile,
mwandishi ameonyesha taswira ya harufu ya damu aliyokuwa nayo Saber alipokwenda
kwa Karima kutaka kumuua baada ya kupandwa na hasira mno.Ukurasa wa 128
mwandishi anasema;
“Saber sasa alishikwa na hasira kali mno za
kuehusha.
Harufu
ya damu ilikuwa kali kwenye tundu za pua yake”.
Vilevile,
mwandishi ametumia misemo mbalimbali. Misemo ni maneno yanayotambulisha
mazingira maalum au kuijulisha hadhira wakati unaohusika katika kazi ya fasihi
inayoshughulikiwa. Mwandishi amemtumia Saber aliyeshindwa kulala usiku kucha
kwa kusema usemi usemao, “kutopata lepe la usingizi”. Ukurasa wa 67 mwandishi
anasema;
“Usiku mwingine pasipo kupata hata lepe la
usingizi”.
Pia,
mwandishi ametumia msemo pale mama Saber alipomwambia Saber akamtafute baba
yake baada ya miaka 30 kupita. Mwandishi alitumia msemo wa “kuchezwa machale”.Ukurasa wa 10;
“kama kwamba nilichezwa
machale na kutambua
yale
amabayo yangetokea”.
Kipengele
kinachofuata ni kipengele cha uhusika na wahusika. Kama vinavyojadiliwa katika
fasihi. Dhana hizi zinafafanuliwa kama ifuatavyo.
Mbunda
msokile (1993) anaeleza dhana ya wahusika kuwa, wahusika ni watu, wanyama, au
viu katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.
Wamitila,
k. w (2002) anaeleza kuwa, wahusika ni viumbe wanaopatikana katika hadithi
yoyote ile. Anaendelea kusema kuwa, viumbe hawa huwa ni sehemu ya kazi nzima .
Kwa
ujumla, wahusika ni jumla ya viumbe wote, vitu ama kitu chochote ambacho
mwandishi au msimulizi amekipa uwezo wa kubeba matendo na kuhakikisha ujumbe
aliokusudia msimulizi au mwandishi katika kazi ya fasihi unafikishwa kwa
hadhira lengwa.
Mwandishi
wa riwaya hii ya Msako amewachora wahusika wake kwa namna tofautitofauti. Hivyo,
katika andiko hili tutaangalia wahusika hawa na jinsi walivyochorwa kuuwakilisha
uhusika wao. Pia, kuna wahusika ambao wanafanana majina, hivyo wahusika hawa
watatofautishwa kwa kupewa namba.
SABER.
Huyu
ni mhusika bapa ambaye habadiliki na hakui kisaoikolojia. Hii ni kutokna na
matendo yake na tabia zake kutobadilika. Mwandishi amemchora mhusika huyu kama;
muuaji, mwizi, mhalifu, hana mapenzi ya
kweli, ni malaya na mhuni. Mwandishi hakuonyesha mabadiliko yoyote ya tabia ya
mhusika huyu. Mwandishi amemchora Saber kama mhusika bapa ili kuonyesha kuwa
katika jamii zetu kuna watu wasiobadika.
SAYED
SAYED EL-REHEIMY (1)
Mhusika
huyu amechorwa kama mhusika mkwezwa. Yuhu ndiye baba yake Saber.Yaani amepewa
sifa na uwezo uliopitiliza ukilinganisha na uhalisi wa maisha yake yalivyo.
Amechorwa kama mtu maarufu, mpenda starehe, tajiri na mwenye hadhi. Mafano (uk
9) mwandishi anaeleza sifa za muhusika huyu.
Mhusika huyu amechorwa kama mtu tabaka kwani amekuwa mwakilishi wa tabaka
la wenye nacho, pia, kama mtu binafsi kulingna na tabia zake alizokuwa
anafanya.
“Yeye ni mtu mwenye kipato kizuri
kabisa. Wakati huo alikuwa mwanafunzi bado, lakini hata wakati huo alikuwa na
uwezo wa kutosha na hadhi.”
SAYED
SAYED EL-REHEMY (2)
Huyu
ni muhusika msaidikzi ambaye dhima yake kubwa ni kuwakilisha dhamira fulani tu.
Hii inajidhihilisha ambapo mhusika huyu anawakilisha tabaka la wenye navyo
wenye kumiliki mali katika jamii. Mfano (uk13)
“ kama tu bahati ingelikuwa upande
wake Sayed Sayed El-Rehemy, mumiliki waduka
la vitabu la el-manshiay.”
SAYED
SAYED EL-REHEIMY (3)
Huyu
ni muhusika msaidizi. Ni mhusika ambaye tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi).
Hivyo, ni mhusika ambaye amewakilishwa dhahili, mhusika tunamtazama kama mtu
tabaka kwani anawakilisha tabaka la wafanyakazi kama madaktari. Yeye huyu ni
dakitari bingwa wamagonjwa ya moyo Cairo. Pia amechorwa kama mtu katili sana kwani, alishindwa kumwonea
huruma Saber (uk. 28) mwandishi anasema;
“kwa
bahati mbaya mimi si mamlaka inayoshughulukia waliopotea”
SHEHE
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la wanadini, kwani anawakilisha kundi la watu wanaoamini
dini na watu wanaoabudu.Mfano, (uk16)
“Shehe ambaye alikuwa ameketi huku
amekunja miguu akiwa katika tafakuri nzito, alisema, “tafuta na utapata.”
BWANA
KHALIL ABDUL NAGA
Huyu
ni muhusika duara. Ambaye huwa anakua kiakili na anabadilikabadilika na ana
sifa kamili za mtu na ana sifa uzuri na ubaya. Ni mhusika ambaye pia
tumemfahamu kwa kusimiliwa na msimulizi (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la watu wenye kipato yaani matajiri na yeye ni miongoni mwa
matajiri wa jijini Cairo. Mhusika huyu ni mmiliki wa Hotel ya Cairo, ni mme wa
Karima, ni mzee kiumri, ameuawa na Saber.
ALY
SERIAKOUS
Huyu
ni mhusika mwenye sifa ya ubapa kwani amekuwa habadiliki wala kukua. Hivyo,
yeye ni kijana mwenye tabia nzuri. Ni mhusika ambaye tumemfahamu kwa kusimiliwa
na msimulizi (maizi) wasifu wake. Vilevile ni mhusika ambaye amewakilishwa
dhahili. Pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la
watu wenye kipato cha chini na wenye kuhangaika na vibarua kila siku. Ni
mchukuzi katika Hotel ya Cairo, ni kibarua wa Khalil, alihusishwa na kifo cha
Khalil, ni kijana mchangamfu na mchapakazi, pia amesingiziwa kesi ya mauaji, ni
mhusika mdogo.
MOHAMED
EL-SAWI
a) Ni
bawabu katika Hotel ya Cairo.
b) Pia
ni mfanyakazi katika Hotel ghiyo.
c) Mshauri
wa karibu wa Khalil.
d) Ni
mzee na anaipenda kazi yake.
e) Alifanya
kazi kwa uaminifu.
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la watu wenye kipato cha chini na wenye kuhangaika na
vibarua kila siku.
ELHAM
a)
Ni mwanamke
mchapa kazi na anafanya kazi katika ofisi za gazeti la sphinx.
b)
Ni mpole na
mwenye huruma.
c)
Ni mchumba wa
Saber.
d)
Hamjui baba
yake.
e)
Ni mwanamke
msomi na anayejitambua.
f)
Ana mapenzi ya
kweli.
g)
Ni mwanamke
mwenye msimamo.
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la wafanyakazi.
KARIMA
a) Ni
mke wa Khalil.
b) Ni
mwanamke asiye na huruma (mkatili).
c) Ni
mwanamke msailiti.
d) Ni
mwanamke ambaye mali zote za Khalil zipo chini yake.
e) Ni
miongoni mwa wauaji Khalil.
f) Ni
mwanamke mwenye tamaa na mali.
g) Ni
mhanga wa mila potofu, kwani aliolewa na mwanaume asiyempenda kwa sababu ya
umaskini.
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu binafsi kwani ni zao
ambalo linaweza kujitokeza kwa namna nyingine tofauti na yeye jinsi alivyo.
IHSANI
TANTAWI
a) Ni
mfanyakazi katika ofisi za gazeti la sphinx.
b) Mwanaume
mwenye huruma.
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la wafanyakazi.
AMR
ZAYED
a) Ni
baba mzazi wa Elham.
b) Alimtaliki
mkewe (mamaye Elham)
c) Ni
msailiti.
d) Mwanaume
aliyeitelekeza familia yake.
Ni
mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu binafsi kwani ni zao
ambalo linaweza kujitokeza kwa namna nyingine tofauti na yeye jinsi alivyo.
Mtagusano,
ni dhana inayorejelea mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi ya
fasihi. Huhusisha mwigo au uwathiriano katika kazi ya fasihi. Mtagusano huweza
kujitokeza katika kipengele cha mandhari ambapo mwandishi hutumia mandhari
ambayo si ya eneo husika lakini anaelezea mambo yanayohusu eneo hilo. Pia
hujitokeza katika kipengele cha lugha ambapo mwandishi hutumia lugha mbili
ndani ya kazi moja yaani inaweza kuwa anatumia lugha ya Kiswahili na wakati huo
huo anatumia lugha ya Kiingereza. Halikadhalika, kipengele hiki hujitokeza
akatika maudhui ambapo mwandishi huonesha maiasha ambayo si halisi katika jamii
anayoiandikia. Wakati mwingine mwandishi anaweza kueleza mambo kwa uwazi kiasi
kwamba yanakwenda kinyume na maadili ya jamii husika. Kwa mfano mwandishi
anaweza kuwa naeleza suala la mapenzi lakini namna alivyoyaeleza ameyaeleza kwa
namna ya uwazi kiasi kwamba anakwenda kinyume na idili na tamaduni za jamii ile
kwa jumala.
Katika
riwaya ya MSAKO mtagusano umejitokeza katika kipengele cha maudhui ambapo
tunamuona mwandishi ameeleza kuhusu mapenzi lakini namna alivyoyaeleza
ameyaeleza kwa uwazi hali inayopelekea kwenda kinyume na maadili ya waafrika.
Jambo hilli hujidhihirisha katika ukursa wa 22, mwandishi anasema;
Hakuna kidokezo cha maongezi yaliyofanyika kandokando ya bahari
Karibu na mitumbwi
iliyobinuliwa chini juu, juu chini. Mazungumzo
Yaliyogubikwa na
mahaba na nyege kali ya ngono.
Neno
‘nyege’ kama lilivyotumiwa na mwandishi linaleta ukakasi katika kulitamka mbele
za watu kwani ni kinyume na maadili ya kiafrika kueleza mapenzi kwa uwazi.
Mwandishi angeweza kutumia mbinu ya ufumbaji ili kuifanya hadhira yake
isijisikie vibaya wakati wa kuisoma kazi husika.
Pia
katika ukurasa wa 47 mwandishi anasema;
‘‘Kila
nitakaposikia hamu ya kufanya hivyo’’, Yule msichna alisema
Walipokuwa hoi
baada ya kufikia mshindo. Alimlalia kwenye matiti
yake,
akiwa hoi katika namna ya kuburudisha.
Katiak
mfano huu maneno, ‘alimlali kwenye matiti’ yanaonesha uelezwaji wa mapenzi kwa
uwazi katika riwaya hii jambo ambalo ni kinyume na idili na tamaduni za
muafrika.
MSUKO
WA VITUSHI
Msuko
wa vitushi ni mtiririko wa mawazo, visa na matukio na namna yanavyopangwa na
kufuatana katika kazi fulani ya kifasihi. Msuko wa vitushi huwa na sifa kadhaa
ambazo hujenga mtirirko wa kazi nzima. Sifa hizo ni kama vile; mjongeo,
usababishina msukumo/motifu. Katika riwaya hii ya Msako sifa hizi zimejitokeza kama ifuatavyo;
Usababishi,
Katika riwaya hii matukio yameweza kujengwa kiusababishi ambapo tukio moja
linasababisha kutokea kwa tukio linguine. Kwa mfano; tukio la kufa kwa mama
yake Suber (Basima Omran) linasababisha tukio la Suber kusafiri kwenda Cairo
kwa lengo la kumtafuta baba yake (Sayed el-Reheimy). Hili lilitokea baada ya
Suber kubaki mpweke bila ya kuwa na ndugu wala rafiki. Hivyo akaona ni vyema
kuanza harakati za kumsaka baba yake na ndicho hasa chanzo cha jina la riwaya
hii. Katika uk…mwandishi anasema;
“Nitaanza maisha mapya huko Cairo,
mbali kabisa na mambo haya huku” “Mungu na airehemu roho yake. Alikupenda mno
kiasi cha kukuharibu kuwezakumudu maisha ya aina nyingine.”
Pia
kitendo cha kutoka Alexandria kwenda Cairo kumtafuta baba yake kinasababisha
Suber kujihusisha kimapenzi na wanawake wawili ambao ni Karinma na Elhamu,
suala ambalo linasababisha kutokea kwa tukio la mauaji ya mzee Khahili Abdul
kwa sababu ya mapenzi. Na tama yakutaka kumiliki mali yam zee huhu. Katika
uk.86, mwandishi anasema;
“Mwenyewe alishangazwa na nguvu ya
pigo lile na matokeo ya kuchefua. Yule mzee alipiga ukulele mdogo halafu
manung’uniko kidogo kasha kimya”
Vilevile
tukio hili la mauaji linamsababishia Suber kuwa na mgogoro binafsi pia
linasababisha ashindwe kuishi kwa amani baada ya kuanza kufuatiliwa na mapolisi
kila alikokuwa akienda na hatimaye anaishia mikononi mwa nguvu ya dola kwa
kutumikia kifungo jela, suala ambalo linahitimisha shughuli nzima ya msako
dhidi ya baba yake mzazi. Pia tukio hili linahitimisha masimulizi mazima ya
hadithi hii.
Sifa
nyingine ni Motifu, hivi ni vitu vinavyosukuma matukio kwenda mbele na kufanya
masimulizi yatoke hatua moja kwenda nyingine. Kuna aina mbalimbali za motifu
ambazo hutumiwa sawa katika kazi za kifasihi, kama vile Motifu ya safari,
ndoto, mizimu, mashetani, majini na motifu ya maji (bahari). Katika riwaya ya Msako, motifu kadhaa zimejitokeza kama
ifuatavyo;
Motifu
ya safari. Msanii hutumia safari za wahusika wake ili kufikisha ujumbe Fulani
alioukusudia kwa hadhira yake. Kaika uk.16-17, safari imejitokeza kupitia
mhusika Suber ambaye anasafiri kutoka Alexandria kwenda Cairo kumtafuta baba
yake. Safari hii ya msako inaibua dhamira ya mapendo. Katika uk.17 mwandishi
ameandika hivi;
“Alexandri ilififia kwa mbali kadri gari moshi lilivyoongeza mwendo
kuelekea Kusini upande wa Cairo.”
Halikadhalika
Motifu ya ndoto/njozi imetumika. Hii huhusisha uwepo wa ndoto au matendo ya
kinjozi ambayo hayapo. Msanii humchora mhusika akiwa katika hali ya ndoto au
njozi. Kwa mfano katika riwaya hii motifu ya ndoto imejitokeza kwa kiasi
kikubwa kuliko aina nyingine za motifu. Katika uk.50 mhusika Suber anaonekana
kuwa katika ndoto juu ya suala la kumpata baba yake. Vilevile katika uk.48-50
kuna ndoto imejitokeza, ndoto ambayo inajenga dhamira ya nafasi ya mwanamke
katika jamii. Katika dhamira hii mwanamke amechorwa kama mtu anayedharaulika.
Motifu
ya maji/ bahari, hutumiwa na mwandishi ili kufikisha ujumbe juu ya mambo ambayo
huweza kuwakumba watu pindi wawapo katika safari za majini. Lakini pia
mwandishi hulenga kuisukuma kazi yake mbele katika hali nzima ya usukaji wa
matukio na vitushi. Katika uk.89 mwandishi anasema;
“Boti ya injini ilikuwa
imemkosakosa nchi chache. Boti yake iliyumbayumba kwa nguvu huku na huko katika
njia yake. Alichukua makasia-bapa na kupiga makasia kurudi mpaka pale
alipochukuliaboti ya kujifurahisha.”
Sifa
nyingine ya msuko ni mjongeo, hii ni namna kazi fulani inavyoanza na kuisha.
Kwa namna nyingine mjongeo hulejelea kazi inaendaje kutoka mwanzo hadi mwisho,
huhusisha mwanzo wa mgagaro, kukua kwa mgogoro, kilele cha mgogoro na hatimaye
mwisho wa mgogoro ambao hutoa sululisho fulani ama zuri au baya.
Katika
riwaya ya Msako kisa kinaanzia pale
anapoambiwa na mama yake kuwa baba yake bado yu hai tofauti na alivyokuwa
amemwambia awali. Na huo ndio unaokuwa mwanzo wa kisa kizima katika andiko
hili. Kisa kinaanza kukuwa baada ya Suber kuamua kusafiri kuelekea Cairo kwa
lengo la kumtafuta baba yake. Kisa kinazidi kukuwa na kufikiafikia kilele chake
pale ambapo Suber amekwishaanza shughuli nzima ya msako huko Cairo, na ndipo
katika harakati zake hizi anaanza kujihusisha na mapenzi na mke wa bwana
Khahili pamoja na binti-Elham. Mwisho wa kisa hiki ni baada ya mhusika Suber
kufanya mauaji dhidi ya bwana Khahili mzee aliyekuwa mmiliki wa hoteli kubwa na
maarufu pale mjini Cairo iliyojulikana kwa jina la Cairo Hotel na tamati kabisa
ya kisa hiki ni kufungwa kwa Suber gerezani/jele
Katika
riwaya hii ya Msako, mianzo na miisho iliyotumika katika riwaya hii ni ile ya
kujirejelea kwa maana simulizi inaanza kwa kuturejesha katika shughuli ya
mazishi ya Basima Omrani ambaye ni mama yake Saber, mfano sura ya kwanza (uk
1);
Kwa macho yenye machozi alitazama kuelekea
kwenye maiti iliyokuwa ikiondolewa kutoka kwenye jeneza na kupelekwa kwenye
kaburi liliokuwa wazi, maiti iliyoonekana kana kwamba haina chembe ya uzito
katika sanda.
Na
baada ya hapo, simulizi inaanza kwa kutuonesha Saber na Basima Omrani, wakiwa
wanazungumza kuhusu msako wa kumtafuta baba yake Saber ambaye ni Sayed Sayed el
Reheimy kama invyojidhihirisha (uk 7-8);
“Nilitambua hilo siku
ile waliponihukumu.” Alikaa kimya kwa mda usio wake ukiwa katika hali ya kukata
tamaa kbisa. “Saber, hii ina maana kwamba huna budi kuniacha,” alisema.
Niende wapi? Aliuliza
akiwa katika hali ya hamaki iliyochanganyika na hasira.
“Kwa baba yako,”
alijibu katika sauti iliyosikika kwa shida.
Alinyanyua kope za
macho yake na kumaka kwa hasira “baba yngu…”
Aliitikia kwa
kichwa.
“lakini amekufa.
Uliniambia alikufa kabla sijazaliwa.”
“Nilikwambia
hivyo. Lakini haikuwa kweli.”
Baba yangu, yu
hai…Haiwezekani… Baba yangu… yu hai.”
Huo
ndio mwanzo wa riwaya hii ya msako jinsi ilivyoanza katika kusimuliwa kwake.
Pia,
miisho iliyotumika katika riwaya hii ni miisho ya kawaida. Kwa sababu simulizi
inatuonyesha Saber akiwa jela baada ya kufanya mauaji ya bwana Khalil kama
inavyoonyeshwa sura ya kumi na moja (uk92);
Bwana Khalil! Amka!
Amka! Bwana Khalil imekaribia saa mbili kamili. Bwana Khalil! Bwana Khalil!
Aliusukuma ule mlango ili kufungua na kwa makini alitazama mle ndani. Bwana
Khalil taratibu. Halafu: “Aah, Mungu wangu bwana Khalil! Bwana! Bwana! Saidia! Saidia! Aly! Aly! Saidia! Bwana
Khalil ameuawa! Polisi! Polisi! Saidia!”
Hatimaye,
baada ya Saber kumuua mzee huyo alikamatwa na kufungwa jela. Simulizi inaishia
kumuonesha Saber akiwa jela akiwa na mwanasheria.
mfano (uk134); Yule mwanasheria alitabasamu kwa kuelewa “kuna tu katika yanayofaa”
Saber alipandisha mabega juu na
kushusha pumuzi.
Aah! Acha lolote nalitokee sasa.
MBINU
ZA KIBUNILIZI
DAYALOJIA
Dayalojia
ni mbinu ambayo mtunzi hutumia majibizano dhidi ya wahusika katika kazi ya
fasihi. Wahusika hupewa maneno na kujibizana waokwa wao. Katika riwaya hii
mbinu hii imetumika kwa kiasi kikubwa kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho kwa
mfano katika uk.12 kuna majibizano kati ya Suber na mchunguzi wa mauaji ya
bwana Khahili, kuna mahojiano kama ifuatavyo;
“Jana uliondoka saa ngapi hapa
hoteleni?”
“Saa
nne asubuhi”
“Uliludi saa ngapi?”
“Baada ya saa sita usiku”……n.k.
Lakinin
pia katika uk.123 kuna mazungumzo kati ya Suber na Aly Seriakous kama
anavyothibitisha msanii;
“Aly seriakous. Hawajampata
mwingine
“Labda alikiri kosa?”
“sijui”
“Aloishawishiwa na wizi uchwara.”
“Aliukana wizi ule.”….n.k.
Mbinu
hii hutumika kwa lengo la kutomchosha msomaji/msikilizaji, lakini pia huonesha
ufundi katika uteuzi wa maneno na kuonesha asilia ya mhusika.
Taharuki,
hii ni hamu au shauku ya kutaka kujua nini kitafuata baada ya tukio ama kitendo
fuani katika hali nzima ya usimulizi wa kazi husika ya kifasihi. Ndani ya
riwaya hii mbinu hii pia imejitokeza kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano simulizi
yenyewe imeisha kwa kutuachia wasomaji taharuki ya kutaka kujua hatima ya Suber
itakua ipi baada kuwa amekamatwa na polisi na kupelekwa katika sheria kuamua ama kufungwa au
kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa baada ya kugundulika kuwa amehusika na kifo cha
mzee Khahil Abdul. Katika uk.146 mwandishi anasema;
“Yule mwanasheria alitabasamu kwa
kuelewa. “Kuna maana tu katika yanayofaa.” Suber alipandisha mabega mabega yake
juu na kushusha pumzi. “Aah! Lolote na litokee sasa.”
Lakini
pia taharuki inajitokeza baada ya Suber kuchukua jukumu la kwenda Cairo
kumtafuta baba yake baada kifo cha mama yake kwa sababu hakuwa na namna ya
kuishi badala yake baba yake ndiye atakayekuwa msaada mkubwa katika maisha
yake. Hali kama hii inaacha maswali kwa wasomaji kwa mfano wanaweza kujiuliza,
je, atafanikiwa kumpata baba yake?, Atakumbana na vikwazo vipi katika msako
huu? Na maswali mengine kadha wa kadha. Kwa mfano katika uk.8 mwandishi
anaonesha suala hili kwa kusema hivi;
“Lakini huenda amekwisha kufa.”
“Au pia yu hai”
“Kwa
hiyo niyapoteze maisha yangu nikimtafuta mtu ambaye hata uwepo wake sina uhakika
nao?
Lakini pia katika uk.64 taharuki
inajitokeza pale ambapo Suber katika utafiti wake anajawa na tatizo la kuanza
kuishiwa pesa ili hali bado hajafanikiwa kumpata baba yake na huko Cairo hana
mtu yeyote anayewaza kumsaidia kiasi cha pesa ili aweze kujikimu. Katika
ukurasa huo mwandishi anabainisha haya;
“Nini
kitatokea endapo fedha zake zitamwishia wakati wowote sasa? Hana wa kumwendea.
Kitu pekee kinachomsukuma ni hofu ya kurudi kwenye maisha yake ya zamani.”
Mbinu
hii hutumika kwa lengo la kumshawishi msomaji aweze kuendelea kufatilia kisa
husika katika kazi Fulani ili apate kujua hatima ni nini, vilevile mbinu hii
huondoa uchovu kwa wasomaji na kuwafanya waendelee kuisoma au kusikiliza kazi
husika ya kifasihi.
UTANZIA
Utanzia
ni mbinu ambayo hutumia vipengele mbalimbali vinavyozua masikitiko, huzuni, na
jitimai kutokana na vitu kama mateso, njaa, vifo, ulemavu, kufungwa jela na
kadhalika. Katika riwaya hii mwanzoni kabisa mwa ukurasa wa kwanza kuna suala la shuguli nzima ya mazishi ya
mama yake Suber (Basma Omran). Suber anaonekana kuwa na machungu sana, vilevile
hata wasomaji au wasikilizaji wa kisa hiki waweza kujawa na hudhuni. Katika
ukurasa huu mwandishi anasema;
“Lakini sasa mazingira ya wakati
huo yalimwamshia hisia kali za uchungu na huzuni na akatamka, “Robo karne ya
hali ya upendo, kubembelezwa, kujali, yote imepotea imemezwa na ardhi kana
kwamba haikuwahi kutokea.”
Vilevile,
mbinu hii imejitokeza pale ambapo mhusika Suber anapofanya mauaji ya kikatili
dhidi ya bwana Khahil kwa kumpiga na mtarimbo kichwani kitendo kinacholeta
huzuni kubwa kwa wasomaji na hata kwa wanajaamii ile pale Cairo hususani
wafanyakazi wa kwenye ile hoteli. Hili limejitokeza katika uk.86, ambapo
mwandishi anasema;
“Mwenyewe alishangazwa na nguvu ya
ajabu ya pigo lile na matokeo yake ya kuchefua. Yule mzee alipiga ukulele
mdogo, halafu manung’uniko kidogo, kasha kimya.
Ufutuhi
na matumizi ya ucheshi, kejeli, ubeuzi, na tanzia. Ni maneno yanayokusudia
kufundisha na kufurahisha. Mfano, Saber alipokuwa anamtafuta baba yake huko
Alexandria alipokuwa maeneo ya marmar alikaribishwa na msichana mmoja. Huyo
msichana alimwambia Saber sikuweza kuja kukupa salamu za rambirambi, lakini
nilisubiri mpaka uje Le Canard. Yule
msichana alimwambia Saber kwa sauti laini, je una mikwamo ya kifedha? Yule
msichana aliendelea kwa namna ya ushawishi
“mtu
kama wewe hawezi kuwa na shida ya fedha” uk 15.
Walipeana
mikono pasipo kusema lolote na kuondoka zake yale maneno ya kule msichana
yalimjia akilini tena, mtu kama wewe huwezi kuwa na shida ya fedha. Hii ni
kejeli au dhihaka. Pia kuna kauli inayofurahisha na kufanya mtu afikirie kuhusu
mwonekano au umbo la hicho kitu uk,19 aya ya pili.
“Yule
msichana alinyanyua kichwa chake na kuonyesha uso wake wenye mikunjo mikubwa na
pua kubwa iliyojikunja kwa mbele.