Jumamosi, 6 Juni 2015

Mashairi ya kiswahili

USHAIRI WA KISWAHILI
HAKI
1          Maisha haya jamani, kweli niipatashika
Maisha kama majani, kweli yanapukutika
Maisha yalo gizani, leo yaanasikika
Haki yamtu jamani, hakika nipatashika.

2          Tuliishi kwaamani, tena kwakujiamini
Haki zetu mikononi, wote tulizitieni
Lakini wetu karani, leo twamzikeni
Haki ya mtu jamani, hakika nipatashika.

3          Kila mnyonge nyumbani, wote walifurahia
Swahibu kwake moyoni, kwake alipigania
Amani kwetu moyoni, wote tulisherekea
Haki ya mtu jamani, hakika nipatashika.

4          Kichwa chake chahekima, busara zimesimama
 Kelo za watu mapema, tayari kuzitazama
Waume na kinamama, haki hawakulalama
Haki ya mtu jamani, hakika nipatashika.

5          Tuliishi kwa matao, busara yake karani
Karani wetu mtwao, sote twaweka kirini
Twakukumbuka wanao, leo hii korokoroni
Haki ya mtu jamani, hakika nipatashika.

6          Mungu ulo mbinguni, sikia hiki kilio
Mjalie wetu karani, korokoroni kilio
Wote tunamdhamini, twomba tena kwakilio
Haki ya mtu jamani, hakika nipatashika.

NA RICHARD, KASHINJE 0764711129

rkashinje@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni